Taarifa Kuhusu HUAWEI Cloud na Faragha
HUAWEI Cloud ni programu inayopakia data ya mtumiaji kwenye seva ya wingu kiotomatiki ili uweze kufikia na kutumia data yako wakati wowote kwenye kifaa chochote kilichoingiwa ndani.
Unapoanza kutumia Cloud, data yako, ikiwemo wawasiliani wako, ujumbe, picha, video, ingizo za rekodi ya nambari za simu, madokezo, rekodi, kalenda, kichujio cha unyanyasaji, mipangilio ya Wi-Fi, na data nyingine ya programu zinaweza kupakiwa na kuhifadhiwa kwenye seva za Huawei. Kipengele hiki kinakuruhusu ufikie data yako baadaye, au kuituma kiotomatiki kwa vifaa vingine kwa kutumia Cloud. Unapoingia ndani kwenye Cloud na kuanza kutumia huduma na usaidizi wake, maelezo yako ya kifaa yakiwemo IMEI, IMSI, na nambari ya modeli yatatumwa kwa Huawei kiotomatiki na kuhifadhiwa.
Ulandanishaji wa Cloud
Unaweza kutumia Cloud kulandanisha kiotomatiki data inayotoka kwa Matunzio, Wasiliani, Kalenda, Daftari, na mipangilio ya Wi-Fi hadi kwenye seva za wingu na vifaa vingine vilivyoingiwa. Badiliko lolote la data kwenye kifaa chako au wingu litazindua ulandanishaji, na kuhakikisha kuwa data iliyoko kwenye kifaa chako inalingana na ile iliyoko kwenye wingu.
Unaweza kuchagua kulemaza ulandanishaji wa kiotomatiki wa programu yoyote ndani ya Cloud na kukomesha upakiaji wa data na ulandanishaji.
Chelezo ya Cloud
Unaweza kutumia chelezo ya Cloud ili kucheleza data iliyoko kwenye simu yako kwenye wingu ili daima uweze kuifikia kutoka kwa kifaa chochote cha Huawei. Ukiwezesha kipengele hiki, data ifuatayo itakusanywa na kuchelezwa kwenye wingu: matunzio, wawasiliani, ujumbe, rekodi ya nambari za simu, rekodi, mipangilio, hali ya hewa, saa, kamera, mbinu za kuingiza, kivinjari, kidhibiti simu, maelezo ya Wi-Fi, ruwaza ya skrini ya mwanzo, na programu. Data inayotoka kwa programu za watu wengine haitochelezwa.
Unaweza kulemaza chelezo ya Cloud ndani ya programu hii wakati wowote ili kukomesha upakiaji wa data.
Data zaidi
Ikiwa umewezesha data ya simu kwa programu zingine, baadhi ya programu hizo zinaweza kutumia hifadhi ya Cloud ili kuhifadhi data na yaliyomo yanayotolewa na Cloud.
Unaweza kulemaza kuchelezwa kwa programu yoyote wakati wowote ili kukomesha upakiaji wa data.
Huawei Drive
Ukiwezesha Cloud, Huawei Drive pia itawezeshwa. Unaweza kuenda kwenye Faili > Huawei Drive na kuhifadhi faili zako za ndani kwenye wingu ili uweze kuzifikia na kuzipakua kutoka kwa kifaa chochote cha Huawei. Lazima uongeze faili kwenye Huawei Drive kimkono.
Usipoongeza faili zozote kwenye Huawei Drive, upakiaji wa data utakomeshwa.
Vipengele vilivyoko hapo juu huenda vikatofautiana kulingana na eneo lako la kijiografia. Rejelea programu halisi ili kupata maelezo haswa.
Kunapohitajika, tunaweza kukutumia taarifa zinazohusu huduma (kama vile notisi za udumishaji wa mfumo, rekodi za miamala, na makumbusho ya matumizi ya hifadhi ya wingu). Unaweza kutokuwa na uwezo wa kuchagua kujitoa ili usipokee taarifa muhimu zinazohusu huduma ambazo hazina asili ya kitangazaji.
Ili kuwacha kutumia Cloud, ni lazima utoke kwa Kitambulisho chako cha HUAWEI. Ili kufanya hivyo, nenda kwenye Mipangilio > Cloud, gusa picha yako ya wasifu na kisha gusa TOKA.