Ukiwa na Swype, uko na uwezo wa kubadilisha kwa urahisi kati ya modi nne tofauti za uingizaji - Swype, Ongea, Andika au Gonga.
-
Swype
Swype ni njia rahisi ya kuingiza maandishi. Hukuwezesha kuingiza neno kwa kuchora herufi. Weka kidole chako kwenye herufi ya kwanza ya neno na uchore njia kutoka herufi hadi herufi, ukiinua baada ya herufi ya mwisho. Swype itaingiza nafasi inapohitajika.
Jifunze zaidi-
Kitufe Cha Swype
Kitufe cha Swype ni kitufe chenye nembo ya Swype. Bonyeza na ushikilie kitufe cha Swype ili ufikie Mipangilio ya Swype.
Kitufe cha Swype kinatumiwa pia kuanzisha ishara nyingi za Swype.
-
Ishara za Swype
Ishara za Swype ni njia za mkato kwenye kibodi za kukamilisha kazi za kawaida kwa haraka. Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
- Kufikia kibodi ya hariri Kufikia kibodi ya Hariri, Swype kuanzia %SWKEICON% hadi kwenye kitufe cha Alama (?123) kwenye kibodi.
- Kufikia kibodi ya nambari Ili kufikia Kibodi ya namba kwa haraka, Swype kuanzia
hadi nambari 5.
- Kuficha kibodi Ili kuficha kwa urahisi kibodi, Swype tu kuanzia kitufe cha Swype hadi kitufe cha Nafasinyuma.
- Zima nafasi otomatiki Finyaza nafasi kiotomatiki kabla ya neno lifuatalo kwa Kupitisha kuanzia kitufe cha Nafasi hadi kwenye kitufe cha Nafasinyuma.
- Kuhariri ukubwa wa neno Badilisha ukubwa wa neno baada ya kuliingiza kwa kugonga neno na kisha kupitisha kuanzia
hadi kwenye kitufe cha Shift
. Orodha ya Chaguo za Maneno zenye chaguo za utumizi wa herufi kubwa itaonekana, inayokuruhusu kuchagua herufi ndogo, kubwa au HERUFI ZOTE KUBWA.
- Vituo Njia rahisi ya kuingiza vituo ni kupitisha kuanzia alama ya swali, koma, nukta, au vituo vingine kwenye kitufe cha Nafasi badala ya kuigonga.
- Teua Zote, Kata, Nakili na Bandika
Teua Zote: Pitisha kuanzia
hadi 'a'
Kata: Pitisha kuanziahadi 'x'
Nakili: Pitisha kuanziahadi 'c'
Bandika: Pitisha kuanziahadi 'v'
- Njia za mkato za programuRamani za Google: Pitisha kuanzia
hadi 'g; kisha 'm'
- TafutaAngazia baadhi ya maandishi na Swype kutoka kwenye
kwenye S ili kufanya utafutaji wa haraka wa wavuti.
- Kubadilisha hadi lugha ya mwisho inayotumiwa.Wakati unatumia lugha anuwai, njia rahisi ya kurudi nyuma kwa lugha ya awali ni Kupitisha kuanzia
hadi kwenye kitufe cha Nafasi.
-
Kuingiza herufi mbili
Kuboresha usahihi wakati unaingiza herufi mbili, chora kwa urahisi au tengeneza mpindo kwenye herufi. Kwa mfano, kupata "aa" katika "baada", chora kwenye kitufe cha "a". Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
-
Kuchagua neno
Kukubali neno msingi lililopendekezwa katika Orodha ya Chaguo za Maneno, endelea na Swyping. Kama sivyo, tembeza kwenye orodha kwa kukokota kidole chako, na kuteua neno unalolitaka. Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
Kuteua maandishi kutoka kwenye orodha, sogeza kidole chako katika mwendo wa mzunguko ili usikilize ingizo za orodha. Mzunguko saa husonga mbele kwenye orodha; kinyume saa husonga nyuma kwenye orodha. Kuinua kidole huondoa ingizo la orodha ya mwisho iliyozungumzwa. Kuchagua neno katika Orodha ya Chaguo za Maneno, telezesha kidole chako juu kutoka kwenye kibodi hadi neno la kwanza katika orodha lisikike, kisha anzisha mwendo wa mzunguko. Kipengele hiki kinapatikana tu wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
-
Kuweka maneno katika herufi kubwa
Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
Weka neno katika herufi kubwa kwa Swyping kidole chako kutoka herufi ya kwanza juu ya kibodi, na bila kuinua, telezesha kidole chako chini hadi herufi ya neno ifuatayo.
Badilisha ukubwa wa neno baada ya kuliingiza kwa kugonga neno na kisha kupitisha kuanzia
hadi kwenye kitufe cha Shift
. Orodha ya Chaguo za Maneno zenye chaguo za utumizi wa herufi kubwa itaonekana, inayokuruhusu kuchagua herufi ndogo, kubwa au HERUFI ZOTE KUBWA.
Kuingiza hali ya CAPS Locj, gonga mara mbili kwenye kitufe cha Shift
.
-
Uwekaji nafasi kiotomatiki
Swype huingiza nafasi kiotomatiki kati ya maneno wakati unapo Swype neno linalofuata katika sentensi. Unaweza kuwasha au kuzima kipengele cha uwekaji nafasi kiotomatiki katika Mipangilio ya Swype.
Uwekaji nafasi kiotomatiki unaweza kuzimwa kwa neno moja kwa Swyping kutoka kwa kitufe cha Nafasi hadi kitufe cha Nafasinyuma.
Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
-
Kubadilisha neno
Badilisha neno kwa kuligonga, kisha teua neno unalotaka kutoka kwa orodha ya Chaguo za Maneno, au angazia neno na Swype neno jipya. Neno jipya litabadilisha lisilo sahihi.
Neno linaweza kuangaziwa kwa kugonga neno na kwa kugusa
au kugonga neno hilo mara mbili.
-
Kuruka kati ya herufi
Wakati mwingine kuepuka herufi wakati wa Swyping huhakikisha unapata neno unalotaka wakati wa kwanza.
Kwa mfano, "aupate" na "aipate" inaweza kuchorwa na njia moja - lakini kumbuka, sio lazima usongee kutoka herufi hadi herufi katika mstari tambarare. Kuepuka "i" wakati swyping kidole chako kwa "p" huhakikisha kwamba neno "aupate" ni ya kwanza katika Orodha ya Chaguo za Neno.
-
Vibambo tofauti
Bonyeza na ushikilie kitufe ili ulete orodha ya vibambo mbadala vya kitue hicho, kama vile herufi kama vile @ na %, na nambari.
Gonga kitufe cha Alama (?123) zitakazopelekwa kwenye kibodi ya Alama.
Kumbuka kwamba vibambo VYOTE vinaweza kuguswa kutoka kwenye kibodi kuu (iwe unaweza kuziona au hapana). Unaweza Kugusa kwa kutumai mwonekano huu wa kibodi, lakini utapata tu maneno ambayo angalau yana namba au alama moja.
-
Kuongeza na kufuta neno
Pitisha kwa makini huongeza maneno yoyote mapya unayoyatumia kwenye Kamusi yako ya Kibinafsi.
Unaweza pia kuongeza neno kwa kuliangazia na kugonga
. Gonga kianzio kinachotokea ili uongeze neno.
Kufuta neno, bonyeza na ushikilie neno katika Orodha ya Chaguo za Maneno, na kisha ugonge Sawa katika kianzio cha uthibitishaji. Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
-
Ubinafsishaji
Swype inaweza kuongeza maneno kwa haraka kwenye kamusi yako kutoka kwa Facebook, Twitter, na Gmail. Kubinafsisha Swype:
- Bonyeza na ushikilie
.
- Chagua Maneno Yangu > Binafsisha kutoka kwenye menyu ya Mipangilio ya Swype
- Chagua kutoka kwenye chaguo za kufanya kubinafsisha na uandike kitambulisho chako.
- Unaweza kubinafsisha Swype kutoka kwa vyanzo vyote.
- Bonyeza na ushikilie
-
-
Ongea
Unaweza kuongea ili uingize maudhui ya maandishi kwa kila kitu kutoka kwa maandishi na ujumbe wa barua pepe kwa visasisho vya Facebook na Twitter.
Jifunze zaidi-
Vituo
Hakuna haja ya kuongeza vituo kwa mikono. Sema tu kituo unachotaka na uendelee. Jaribu hii:
- Bonyeza kitufe cha sauti na uanze kuongea.
- Unachosema: Chakula cha jioni kilikuwa kitamu alama ya mshangao
- Unachokipata: Chakula cha jioni kilikuwa kitamu!
-
Uingizaji wa sauti haupatikani kwenye baadhi ya kibodi
-
-
Andika
Unaweza kutumia kidole chako kuchora herufi na maneno na Swype itaibadilisha kuwa maandishi. Sasa unaweza kuchora herufi kuanzia kushoto hadi kulia au juu ya kila moja. Bonyeza ABC / 123 ili kubadilisha kati ya hali ya herufi na alama.
Jifunze zaidi-
Wezesha mwandiko wa mkono
- Bonyeza na ushikilie
na utelezeshe kidole chako kwenye ikoni ya mwandiko wa mkono.
- Chora herufi kwa kutumia kidole chako kwenye eneo la mwandiko wa mkono.
- Gonga upau wa nafasi kati ya kila neno
- Bonyeza na ushikilie
-
Ishara ya Mguso Anuwai
Ishara ya mguso anuwai hukuwezesha kukamilisha kazi rahisi, kama vile kuweka neno au herufi kuwa kubwa.
- Chora baadhi ya herufi ndogo kwenye pedi ya kuchora
- Baada ya kuingiza vibambo, telezesha vidole viwili juu kwenye eneo la kuandika
- Kipengele cha mwandiko wa mkono kitagundua ishara ya mguso anuwai na kuweka herufi kubwa
-
Mwandiko wa mkono haupatikani kwenye baadhi ya kibodi.
Kipengele hiki hakipatikani wakati huduma ya ufikiaji mfumo wa Explore-by-Touch imewashwa.
-
-
Gonga
Aina ya kawaida ya kuingiza kibodi kwa mikono. Uingizaji wa gonga kwenye kibodi ya Swype hufanywa rahisi zaidi na bora zaidi na baadhi ya vipengele muhimu:
Jifunze zaidi-
Usahihishaji wa Ucharazaji wa Kimakosa
Sio lazima ugonge kila herufi kwa usahihi. Jaribu uwezavyo na Swype itatoa mapendekezo ya maneno.
-
Ukamilishaji Neno
Swype inaweza pia kukisia neno lako wakati unapogonga maneno machache tu.
-
-
Lugha
Kubadilisha lugha kutoka kwenye kibodi: Bonyeza na ushikilie upau wa nafasi. Teua lugha yako unayotaka kutoka kwa menyu ya ibukizi.
-
Swype Connect
Swype Connect hutuwezesha kuwasilisha visasisho na vitendaji muhimu kwenye kifaa chako! Wakati Swype Connect itafanya kazi kwenye 3G, tunapendekeza kutafuta muunganisho wa WiFi kila wakati.
Jifunze zaidi-
Vipakuzi vya lugha
Kuongeza lugha za ziada kwenye Swype ni rahisi:
- Bonyeza na ushikilie
na uteue lugha.
- Kutoka kwenye menyu ya Lugha, teua Pakua lugha.
- Bofya kwenye lugha na upakuaji wako utaanza kiotomatiki.
- Bonyeza na ushikilie
-
Swype Connect haipatikani kwenye kibodi zote.
-
-
Msaada zaidi
Kwa msaada zaidi wa kutumia Swype, tazama Mwongozo wa Mtumiaji wa Swype na Vidokezo vya Swype na Video katika www.swype.com, au kagua Mdahalo wa Swype mtandaoni katika forum.swype.com.